Matokeo ya mtihani wa kitaifa ya mwaka 2021 wa shule zinazofunza masomo ya dini ya kiislam yaani Intergrated schools yametangazwa rasmi leo,huku Aisha Yusuf Mohamed kutoka shule ya Al-Ameen Academy kutoka Nairobi akiubuka bora kwa alama 569.

Nafasi ya pili kitaifa imenyakuliwa na Zakariya Adan Madey akiwa na alama 557 kutoka shule ya Umar Faroq naye Nawal Feisal Abdile kutoka Nairobi Muslims Academy akiibuka wa tatu kwa alama 553.

Akitangaza matokeo hayo hapa jijini Mombasa,mwenyekiti wa kitaifa wa mtaala wa masomo ya dini sheikh Hassan Sugow ametaja kuwa wasichana wamefanya vyema ikilinganishwa na wavula.

Aidha,katika mtihani huo somo la Qurani limetajwa kuongoza,huku somo la lugha ya kiarabu likishika mkia.

Shule ya Al-Hilal Intergrated kutoka Garissa ndio imeibuka ya kwanza kwa alama jumla 516,ikiufuatwa na Bukhari B Intergrated kutoka Wajir ikiwa na alama jumla ya 487.78,Nurul Azhar Academy 482.86,Rahma Academy 462.20 na Bukhari A Intergrated ikiwa na alama jumla 458.

Al-Bukhari A Intergrated imeongoza katika somo la Quran kwa alama ya 83.04, Al-Hilal Intergrated imeongoza katika somo la kiarabu,Fiqh,Hadith na sera,huku shule ya Nurul Azhar Academy ikongoza katika somo la Tawheed.