Mashirika ya kutetea haki za binadamu ya pwani yamekemea kadhia ya baadhi ya wanasiasa wanaosababisha vurugu wakati huu wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu.

Mratibu wa mashirika hayo katika kanda ya pwani Nicholas Songora amesema siasa za Pwani zimeanza kuwa na fujo ambapo zinasababisha ukosefu wa usalama na Amani .

Mashirika haya yamezitaka idara mbalimbali kama vile Tume Huru ya Uchaguzi na mipaka ya IEBC na mengineyo katika serikali kuweza kueka mikakati ya kuhakikisha kuwa kunakuwa na kampeni za Amani.

Neyla Abdallah kutoka shirika la Sisters for Justice amewahusia wanasiasa kujizuia kutoa maneno ya uchochezi ili kuepukan na vurugu.

Amewashauri vijana kutotumika na wanasiasa kwa sababu siasa ni za msimu na Amani ndio muhimu kwa wananchi.

Afisa wa dharura katika shirika la MUHURI Francis Auma amesema iwapo idara hizo za usalama hazitachukua hatua hawana budi kufikisha lawama zao kotini au popote ambapo wataweza kupata usaidizi.

Hivi karibuni visa kadhaa vya vurugu vimeshuhudiwa katika kampeni huku watu wakipoteza maisha yao na wengine wakijeruhiwa .