Serikali imehakikisha kuwa hakuna kisa chochote cha homa ya nyani yani Monkeypox nchini na ukanda wa Afrika Mashariki.

Katibu Mkuu katika wizara ya afya Susan Mochache amesema kuwa serikali imeongeza ufuatiliaji wa virusi vya ugonjwa huo katika maeneo ya kuingia humu nchini.

Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), visa vilivyothibitishwa vya homa ya nyani vimegunduliwa nchini Australia, Ubelgiji, Kanada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Uholanzi, Ureno, Uhispania, Uswidi, Uingereza na Marekani.

Wataalamu wa afya wanasema ukaribu na mtu aliyeambukizwa ni njia moja ya kueneza virusi vya homa hio.

Vile vile maambukizi yanaweza kutokea baada ya kuathiriwa na ngozi iliyopasuka, kamasi, matone ya kupumua, maji ya mwili yaliyoambukizwa au hata kugusa nguo iliyoambukizwa.