Mali yenye thamani isiyojulikana yakisiwa kuharibika baada ya moto kuzuka katika duka moja la kuuza simu katikati mwa jiji la Mombasa.

Chanzo cha moto huo bado hakijabainika huku wazima moto wakifika katika eneo hilo kudhibiti hali.

Moshi umeanza kuonekana mapema leo asubuhi ukitoka katika duka hilo la simu lililoko katika mzunguko wa Fontanella kati ya barabara ya Kenyatta na Moi mjini Mombasa.

Hakuna mali ambayo imeweza kuokolewa kutokana na moshi uliokuwa umejaa ndani ya duka hilo.