Mgombea ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amemkashifu naibu wa rais William Ruto kutokana na kauli yake kuwa ataregesha utendakazi wa bandari ya Mombasa kwa wakaazi wa pwani.

Akizungumza hapa Mombasa Nassir amesema kuwa naibu rais William Ruto alikuwa mstari wa mbele kupinga matakwa ya wakaazi wa Mombasa wakati serikali inapanga kuhamisha utendakazi huo na kuchangia msukumo wa uhamisho huo.

Amesema kuwa naibu rais alifanya hivyo licha ya baadhi ya viongozi wa pwani akiwemo gavana Hassan Ali Joho miongoni mwa viongozi wengine wa pwani kupinga uhamisho huo kupelekwa mjini Naivasha.

Nassir aidha amesema kuwa kinara wa ODM Raila Odinga ndiye atakayerudisha utendakazi wa bandari ya Mombasa , na sio ya Ruto.

Ikumbukwe kuwa Raila Odinga kurudisha utendakazi wa bandari ya Mombasa katika siku mia moja za kwanza atakapochaguliwa kuwa rais wa taifa hili ili kuhakikisha ajira kwa wakaazi wa pwani katika bandari ya Mombasa KPA zinapatikana.