Huenda tatizo sugu la Taka kaunti ya Mombasa likazikwa kwenye kaburi la sahau.

Hii ni baada ya mgombea wa ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir kupania kuleta ujenzi wa mradi wa kiwanda cha kubadilisha taka ziwe ni zenye kuleta manufaa katika jamii badala ya kutupwa kiholela.

Akiwahutubia wazee,vijana na akina mama katika ukumbi wa kanisa la kikatoliki la Mbungoni eneo bunge la Nyali, Nassir amesema kuwa takataka zinao uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme na hata mbolea,hali ambayo anasema itaimarisha uchumi wa kaunti ya Mombasa na hata kuleta manufaa kwa jamii ikiwemo kutengeneza nafasi za ajira.

Kadhalka Nassir ameeleza mbali na kuzalisha nishati na mbolea,mradi huo pia utawezesha hali ya mazingira katika maeneo mbali ya hapa Mombasa kuwa safi na salama.