Huenda ugumu wa upatikanaji wa maji safi kwa wakaazi wa mitaa ya mabanda kaunti ya Mombasa ukapata suluhu.

Hii ni baada ya mgombea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir kuahidi kuweka miradi ya mitambo ya kusafisha maji chumvi kuwa safi katika mitaa ya mabanda iliyoko ndani ya kaunti ya Mombasa.

Akizungumza na wakaazi wa mtaa wa Kaachonjo Wadi ya Tudor Nassir amesema kuwa mradi huo utaleta afueni zaidi kwa wakaazi wanaoishi katika mitaa hiyo ambao wanatumia maji ya visima ambayo ni ya chumvi

Vilevile amewaomba wakaazi wa mitaa hiyo kudumisha Amani pindi tu mradi huo utakapo wafikia.

Wakati huo huo Nassir amesema atafanya mpango ili kuona kuwa mitaa ya mabanda kaunti ya Mombasa inaboreshwa.