Aliyekuwa makamu wa rais Kalonzo Musyoka ametangaza kurejea katika muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya wa Raila Odinga.

Kalonzo ametangaza hayo Alhamisi baada ya kukutana na maafisa wa chama cha Wiper.

Amesema amegundua kuwa mustakabali wa taifa ndio muhimu,hivyo kuahirisha ndoto zake za kugombea katika uchaguzi wa Agosti.

Kalonzo amesema baada ya mashauriano mapana ameamua kukubali kwa unyenyekevu uteuzi wake katika Azimio.

Mwezi uliopita Kalonzo aliachana na Azimio na kutangaza azma yake ya kuwania urais.Hii ilikuwa baada ya mgombea urais wa Azimio Raila Odinga kumchagua kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua kama mgombea mwenza wake mbele ya bosi wa wiper.