Bunge la kaunti ya Kwale limepitisha mswada wa kumng'atua afisini karani wa bunge hilo kwa madai ya ufujaji wa fedha za umma mwaka 2020 .

Wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya fedha bungeni humo Patrick Mangale wameeleza kukosa imani na karani huyo daktari Hamisi Dzila kwa kutumia fedha za umma kinyume cha sheria.

Hapo awali karani huyo alitimuliwa afisini kisha kurudishwa kazini baada ya amri ya mahakama.

Dzila aliyetarajiwa kufika mbele ya kamati hio hii leo kuhojiwa bali hakutimiza agizo hio.