Wananchi katika eneo la Ndigiria kaunti ndogo ya Ganze wamelalamikia kuhangaishwa na ndovu.

Wakiongozwa na kiongozi wa maswala ya kijamii karisa Nyiro,wananchi hao wamesema kuwa ndovu hao wanaharibu mimea mashambani mwao.

Kuligana na Nyiro,wananchi pia wanaogopa kurauka kwa shuhuli zao za kila siku kwa kuogopa kuvamiwa na ndovu hao.

Wananchi hao sasa wanawataka maafisa wa kws kuingilia kati ili kuwafurusha ndovu hao.