Familia moja kutoka eneo la Mkilo Mariakani gatuzi dogo la Kinango kaunti ya Kwale inalilia haki baada ya mpendwa wao kutekwa nyara na watu wanaoaminika kuwa maafisa wa polisi.

Omar Chidoti Mangale mwenye umri wa miaka 33 na ambaye ni imamu na ustadhi wa madrassatul Madina Mariakani alichukuliwa katika hali tatanishi siku ya Ijumaa tarehe 20 na watu wanaoaminika kuwa maafisa wa polisi nyumbani kwake anakoishi huko Mariakani Juma Ismael ni kakake Omar.

Zainab Chengo Mohammed ambaye ni mke wa Omar Chidoti amesema kuwa mumewe alikamatwaa pamoja na Kassim Musa lakini badaye wakamuachilia kijana huyo na kuitaka serikali kuwasaidia kujua mpendwa wao aliko.

Kulingana na Mangale Chidoti Chondo ambaye ni baba ya Omar ni kwamaba tangu siku hiyo hawajapata habari yoyote kumhusu kijana wao licha ya kumsaka katika vituo tofauti vya polisi hata makao makuu ya upelelezi na kuongezea kwamba mtoto wake hajawahi husishwa na mambo ya kihalifu tangu utotoni mwake.

Kwa upande wake afisa wa maswala ya dharura katika shirika la kutetea haki za bianadamu la HAKI Africa Alexander Mbela, ameitaka serikali kuweza kufichua aliko jamaa huyo ili familia hiyo ipate haki.

Kadhalika ameitaka serikali kukomesha visa vya watu kutoweka kwa njia za kutatanisha akidokeza kwamba tangu Januari mwaka huu kufikia sasa ni visa 15 vilivyoripotiwa.