Jumla ya wanawake 50 waliokuwa wamejifungua na kushindwa kulipia madeni ya huduma ya matibabu katika Hospitali kuu ya mafunzo ya rufaa ya ukanda wa Pwani wameruhisiwa kuondoka.

Hii ni baada ya mgombea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir kugharamikia madeni yao.

Wanawake hao aidha ni kwa muda mrefu wamekuwa Hospitalini humo wakihudumiwa kwa matibabu tangu muda wa kujifungua kwao.

Licha ya wao kumaliza huduma zao za matibabu hawakuruhusiwa kuondoka.

Mwanahabari wetu aliyezuru eneo hilo amedokeza kuwa wanawake hao walizua rabsha kwenye lango la kutokea wakiashiria kuchoshwa na muda waliokaa Hospitalini humo.

Hata hivyo licha ya Nassir kuwalipia madeni yao vile vile aliwahakikishia wanapata usafiri wa kuwafikisha nyumbani kwao.