Mgombea wa ugavana wa Kwale kupitia chama cha ODM Profesa Hamadi Boga amemteua aliyekuwa katibu katika idara ya utawala na utumishi wa umma kaunti ya Kwale Nurrein Mwatsahu kuwa naibu gavana wake.

Kulingana na Boga Mwatsahu atachukua nafasi ya Safina Kwekwe aliyekuwa amemteua hapo awali.

Haya yanajiri baada ya Kwekwe ambaye ni katibu katika idara ya magereza nchini ombi lake la kujiuzulu kukataliwa.

Kwa upande wake Kwekwe amesema kuwa ameamua kujiondoa baada ya wapinzani wao kutishia kuelekea mahakamani kupinga uteuzi wake.

Hata hivyo Kwekwe ameahidi kumuunga mkono Boga katika azma yake ya kuwania ugavana wa kaunti hiyo kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9.