Mgombea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Sharif Nassir ametoa wito kwa serikali za kaunti kuondoa ada ya ardhi inayotoza katika sehemu za ibada.

Akiwahutubia waumini katika kanisa la Siloam Ministry wadi ya Mtopanga eneo bunge la Kisauni, Nassir amesema kuwa si jambo la busara kuona serikali za kaunti zinatoza ada ya ardhi kwa sehemu za ibada.

Nassir ambaye alikuwa ameandamana na mgombea mwenza wake Francis Thoya ameahidi kuondoa ada hizo pindi tu atakapochukua uskani wa kuiendesha serikali ya kaunti ya Mombasa.Kulingana naye serikali ya kaunti itakuwa ni serikali inayojali utu na maslahi ya wakaazi.