Polisi hapa Mombasa wanalaumiwa kufuatia kukithiri kwa visa vya mauaji ya kiholela kwa wanabodaboda.

Hii baada ya Bodaboda mmoja eneo la Mtongwe kupatikana ameuawa kwa njia tatanishi na mtu anayedaiwa kuwa afisa wa polisi.

Albert Wekesa ambaye ni mfanyikazi katika sekta ya Bodaboda eneo la Mtongwe,inadaiwa kuwa alikujiwa mwendo wa saa moja usiku nyumbani kwake Mtongwe na mteja wake ambaye alikuwa ni afisa wa polisi aliyekuwa akimbeba kila siku na kumpeleka kazini.

Inasemekana kuwa Albert siku hiyo aliyokujiwa na mteja huyo hakurudi tena ila kilichojiri kesho yake Albert alipatikana amechinjwa na kuuliwa kinyama.

Wakizungumza walipoitembelea na kuifariji familia ya Albert huko Mtongwe ambayo ilikuwa na majonzi kwa kumpoteza mpendwa wao,Mgombea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir,mwaniaji kiti cha uwakilishi wa kike kaunti ya Mombasa Zamzam Chimba Mohammed pamoja na mbunge wa eneo hilo la Likoni Mishi Juma Mboko wamewalaumu baadhi afisa wa polisi kwa kuendeleza maadhila hayo na kumtaka waziri wa usalama wa ndani daktari Fred Mating'i kuingilia kati na kuwafuta kazi maafisa wanaoendeleza matukio ya mauaji ya watu wasiokuwa kuwa na hatia.

Aidha wamesema kuwa watalifuatilia suala hilo hadi pale haki ya mwendazake itakapopatikana.

Kulingana nao ni kuwa Albert alikuwa ywaendelea na kesi,kabla ya kuuliwa kwake alishuhudia tukio lengine la afisa huyo akifanya tukio lengine la mauji,hiyo ikawa chanjo cha mauaji yake.

Mshukiwa hata hivyo alikamatwa na kuzuiliwa huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Mwili wa mwendazake unatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumatatu hadi nyumbani kwao Bungoma kwa mazishi.