Baadhi ya wagombea wa viti vya ubunge kwa chama cha ODM hapa Mombasa wamewasilisha karatasi zao katika zoezi la kupiga msasa wagombea linaloendeshwa na tume ya IEBC katika vituo mbali mbali kote nchini.

Wakizungumza baada ya kuwasilisha makaratasi yao na kuthibitishwa na kuwania viti vyao na tume hiyo ya IEBC hapa Mombasa Mbunge wa Jomvu Badi Twalib na mwenzake anaye gombea kiti hicho eneo la Nyali Said Abdallah wametoa wito kwa wakaazi wa kaunti ya Mombasa ya Mombasa kuwachagua viongozi wa ODM kuanzia ngazi ya juu ya urais hadi ya uakilishi Wadi.

Ni wito uliongwa mkono na mgombea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir akisema mfumo huo utarahisisha utekelezaji wa huduma mbali mbali kwa wananchi.

Nassir anatarajiwa kuwasilisha karatasi zake kwa tume ya IEBC tarehe 6 mwezi Juni.