Mgombea wa wadhfa wa useneta kaunti ya Mombasa kwa tiketi ya chama cha UDA Hamisi Mwaguya amehimiza wakaazi wa kaunti ya Mombasa kushiriki kwenye siasa za amani.

Mwaguya amewasihi vijana kutokubali kutumika na wanasiasa kwa malengo mabaya.

Mwanasiasa huyo aidha amewataka wakaazi wa kaunti ya Mombasa kumpigia kura kwenye uchaguzi mkuu ujao, akiahidi kuwatumikia kulingana na katiba pamoja na kupigania kuregeshwa kwa huduma za bandari ya Mombasa.

Ameyasema hayo baada ya kuidhinishwa na tume huru na ya kuratibu mipaka nchini IEBC kuwania wadhfa huo.

Mwandishi: Ibrahim Juma Mudibo