Wizara ya afya imetangaza kuwa watu 91 wamepimwa na kuambukizwa COVID-19 kutoka sampuli 2,371 zilizopimwa katika saa 24 iliyopita.

Idadi hio inaashiria kiwango cha maambukizi cha asilimia 3.8.Kutoka kwa visa hivyo, 45 ni Wakenya huku 46 wakiwa wageni; 58 ni wanaume na 33 ni wanawake.

Mgonjwa mdogo ana umri wa miaka 5 na mkubwa ana miaka 77.Nairobi imenakili visa 82, Mandera 4, Mombasa 2, Kwale, Nyeri na Siaya kesi 1 kila moja.

Wagonjwa 63 walipona ugonjwa huo, wote kutoka katika Mpango wa Huduma ya Majumbani na Kutengwa.