Chama cha ODM kimemteua Mohammed Mwamkale kugombea kiti cha ubunge Rabai.

Mohammed ni nduguye aliyekuwa mbunge wa eneo hilo William Kamoti aliyefariki kwenye ajali ya barabarani hapo juzi.

Mwenyekiti wa chama hicho cha ODM kaunti ya Kilifi Teddy Mwambire amesema hatua hiyo ni njia moja wapo ya kuendeleza uongozi mzuri wa mwendazake.

Teddy amesema uamuzi huo umechukuliwa na chama na akawaomba wananchi wa Rabai kumuunga mkono mgombea huyo.