Upepo mkali unaotokana na mvua inayonyesha umesababisha hasara baada ya paa la nyumba moja kung’olewa katika mtaa wa Muhajirina Majengo mapya huko Likoni.

Kung’olewa kwa paa hilo kumetatiza shughuli za wafanyibiashara waliokuwa wamekodi katika nyumba hiyo ambayo pia umeme umekata.

Paa hilo lililokuwa limefunga barabara inayotumiwa na wapiti njia, bodaboda na magari limeondolewa na wakaazi wa mtaa huo. Aidha hakuna aliyejeruhiwa katika kisa hicho.