Wizara ya afya kaunti ya Kwale imethibitisha ongezeko la saratani ya kizazi miongoni mwa watoto wakike wenye chini ya umri wa miaka 25.

Afisaa anayeshughulikia afya ya uzazi Kwale Edward Mumbo amesema kwamba hali hio imechangiwa pakubwa na ngono za mapema miongoni mwa wasichana wenye umri mdogo.

Hata hivyo amewataka wazazi kuwapeleka watoto wao kwa uchunguzi ili waweze kuanza matibabu mapema.