Mgombea wa wadhfa wa ubunge wa Mvita Said Twaha amesisitiza kwamba kuna haja ya jamii ya watu wenye walemavu kushirikishwa kikamilifu katika mchakato wa maendeleo.

Mwanasiasa huyo amesema ataandaa vikao na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali katika eneo la Mvita ili wawasajili walemavu watakaoshirikishwa katika shughuli za kimaendeleo.

Akizungumza eneo la Makande Twaha amesema walemavu ni wanadamu kama wanadamu wengine na ni sharti kushirikishwa kikamilifu katika miradi ya maendeleo.