Mgombea kiti cha ugavana wa chama cha Wiper kaunti ya Machakos Wavinya Ndeti amepata afueni baada ya IEBC kutupilia mbali ombi lililotilia shaka uhalali wa shahada yake.

Kamati ya Tume ya IEBC ya Kusuluhisha Mizozo imesema haina mamlaka ya kuthibitisha uhalisi wa shahada hiyo.

Wapiga kura wawili wa Machakos, Gideon Ngewa na Kisilu Mutisya walitaka kamati hiyo kubatilisha kibali cha Ndeti wakidai kuwa hana sifa ya kuwania kiti cha ugavana.

Walikuwa wamedai kuwa vyeti vyake vya masomo vinatia shaka na havilingani kwani hakuna rekodi yoyote ya yeye kujiandikisha nchini Uingereza.