Mwaniaji wa kiti cha ugavana Nairobi Johnson Sakaja ameidhinishwa na Kamati ya Kusuluhisha Mizozo ya IEBC kuwania kiti hicho kwenye uchaguzi wa Agosti.

Hii ni baada ya kamati ya kusuluhisha mizozo ya IEBC kutupilia mbali ombi lililopinga uhalali wa shahada yake.

Kamati hiyo imesema haina mamlaka ya kubainisha uhalisi wa waraka huo.

Mlalamishi, Dennis Wahome, aliiambia kamati katika hati ya kiapo kwamba shahada ya Sakaja kutoka Chuo Kikuu cha Timu nchini Uganda ilighushiwa.