Wadi ya Timbwani eneo bunge la Likoni imetajwa Wadi pekee iliyoandikisha idadi ya juu ya watu waliojisajili kama wapiga kura kati ya wadi zote kaunti ya Mombasa ikiwa na ya jumla ya idadi ya sajili ya watu Elfu 33.

Haya ni kwa mjibu wa mgombea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff.

Akizungumza na wakaazi na waratibu wa timu ya ODM katika uwanja wa shule ya upili ya Timbwani eneo bunge la Likoni Nassir amewataka wakaazi kaunti ya Mombasa kujitokeza ifikapo siku ya kupiga kura kwa viongozi wa ODM ili kuandikisha ushindi wa juu zaidi wa kura kwa chama hicho huku akidokeza kuwa hakuna Wadi kaunti ya Mombasa iliyo na idadi kubwa ya sajili ya watu waliojiandikisha kuwa wapiga kura kama Wadi ya Timbwani.

Nassir ambaye anaazimia kurithi kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa amesema kuwa endapo atafaulu ,katika Siku zake za kwanza baada ya kuapishwa ataweka watumishi wa umma mashinani kupitia mpango wa serikali mitaani ilikurahisisha huduma kwa jamii zilizopo vijijini.

Wakati huo huo Nassir amewashtumu vikali viongozi wa muungano wa kenya kwanza kwa madai kuwa wanaendeleza siasa za uongo kwa wakaazi wa pwani.

Hii nikufuatia mjadala wao wa kutaja uwiano baina ya rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga maarufu Handsheki kwamba ndio chanzo kikuu cha kupanda kwa gharama ya maisha nchini

Aidha Nassir sasa anawaomba wakaazi wa kaunti ya Mombasa kujiweka kando na siasa za uongo akidokeza kuwa Handsheki ililetwa ili kukomesha kushuhudiwa kwa matukio ya vurugu na umwagikaji damu nchini kinyume na muungano huo unavyofikiria.