Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Lamu Issa Timamy amewakosoa viongozi wa sasa wa kaunti hiyo akisema wanatumia utoajai hati miliki kama njia ya kujitafutia umaarufu wa kisiasa kwa wananchi.

Timamy amesema hati miliki za mashamba yaliyopimwa tangu serikali iliopita hazikutolewa hadi sasa wakati uchaguzi umekaribia ndio zinatolewa kama njia ya kuwahadaa wananchi ili waweze kuwapigia kura.

Amesema hatimilkii za mashamba ni haki ya kikatiba kwa kila mwananchi na wala swala ukosefu wa hatimiliki za mashamba kwa wakaazi wa Lamu halipaswi kutumiwa kisiasa.

Aidha amesema nyingi ya hatimiliki zinazotolewa ni maeneo ya mijini pekee huku wamiliki wa mashamba wakiwa hawana hatimiliki licha ya kuwa hayo ndio muhimu zaidi kwa shughuli za ukulima.

Amesema endapo atachaguliwa kuwa gavana katika uchaguzi mkuu ujao atahakikisha mashamabo yote yanapimwa na watu wanapewa hatimiliki za mashamaba yao na wala sio mijini pekee.