Itakuwa vyema endapo kutakuwa na jopo maalum la kufuatilia mienendo ya wanasiasa msimu huu wa kampeni ili kuwadhibiti na kuwazuia kuchochea wananchi kwa kutaka kutimiza malengo yao ya kisiasa.

Haya ni maneno ya kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti ya Lamu na ambaye ni mwakilishi wa wadi ya Kiunga Abdallah Aboud maarufu Baabad.

Aboud amesema kiongozi yeyeto wa kisiasa atakayechochea wananchi anapaswa kupokonywa tiketi yake ya chama hata kama tayari ameidhinidshwa na tume ya IEBC.

Zaidi amesema kiongozi mwenye kuchochea wananchi hana malengo kwa jamii hivyo basi hapaswi kupewa nafasi yoyote ya uongozi.

Amewataka viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Lamu na taifa zima kwa jumla kuuza sera zao kwa wananchi kwa njia ya amani ikizingatiwa kuwa kura ni siku moja na kuna maisha baada ya kura.