Kufuatia ongezeko kwa unyanyasaji wa raia wa kenya wanaofanya kazi katika mataifa ya mashariki ya kati, serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kwamba wanaokwenda katika mataifa hayo hawadhalilishwi.

Akizungumza katika kongamano la wafanyikazi lililoandaliwa hapa Mombasa, waziri wa leba Simon Chelugui amesema kuwa serikali ya kenya na ile ya Saudi Arabia zinashirikiana ili kuhakikisha wakenya wanaokwenda taifa hilo wako salama.

Chelugui amesema serikali imetenga shilingi milioni 70 ili kuhakikisha ujenzi wa nyumba hio katika mji wa Riyadh nchini Saudi Arabia.

Vile vile amesema kua serikali imeweka mikakati ya kutoa mafunzo kwa wafanyikazi walioko katika nchi za nje kujifunza kuhusu haki zao kama wafanyikazi.

Akizungumza katika kongamano hilo mratibu wa serikali ukanda wa pwani John Elung’ata amesema kuwa serikali inapanga mikakati ya kuweka nafasi za ajira humu nchini ili kupunguza idadi ya wakenya wanao safari nchi za nje kutafuta ajira.