Kumekuwa na kizaazaa katika steji ya Matatu mjini Kilifi baada ya viongozi wa makanga kuanza kuwanasa na kuwaosha makanga ambao hawaogi.

Viongozi hao wamesema kuwa baadhi ya makanga wamekuwa wakisusia kuoga na kutatiza abiria kutokana na harufu ya uvundo kutoka kwa nguo na miili yao.

Hamis Kazungu mmoja wa viongozi hao amesema kuwa wamechukua hatua hiyo ili kuhakikisha kuwa makanga hao wanadumisha usafi.

Hatua hiyo inajiri baada ya abiria kulalamikia usafi duni miongoni mwa makanga hao.