Baadhi ya viongozi wa muungano wa Azimio wakiongozwa na gavana wa Kitui Charity Ngilu wamezuru kaunti ya Kwale kumpigia Dede mwaniaji wa urasi Raila Odinga kuwa rais uchaguzi ujao mwezi Agosti.

Viongozi hao akiwemo Naomi shaban, Mishi mboko na wengine kwa pamoja wameunga mkono hatua ya viongozi wanaogombea nyadhfa moja katika eneo moja kuzungumza na kukubaliana kuwa na mwakilishi mmoja atayewakilisha muungano wa azimio.

Wameitaja hatua hiyo kama mbinu bora ya kuhakikisha muungano huo unashinda nafasi zaidi za uongozi katika uchaguzi ujao.

Kutokana na hayo wameahidi kufanya mazungumzo na viongozi wanaowania nafasi moja ili kukubaliana na kuwa na mpperusha bendera mmoja wa muungano wa azimio.

Katika nafasi ya mwakilishi wa kike muungano huo wa azimio una wagombea watatu Fatuma Masito wa Odm, Nimusimu Mwasina wa DAP-K na Husna Shee wa Udm na katika nafasi ya ugavana ni Hamadi Boga wa Odm na Chirau Ali Mwakwere wa Wiper.

Wakati huo huo viongozi hao wamemtaja Raila kama mkombozi wa taifa kutoka kwa ufisadi na unyakuzi wa ardhi, huku wakimtaja kuwa kiongozi pekee atakayeleta maendeleo nchini.