Muungano wa madiwani wa zamani humu nchini unalalamikia ucheleweshwaji wa marupurupu na pesa zao za uzeeni takriban shilingi milioni 1.5.

Wameeleza kuwa mwaka 2016 bunge la seneti lilipitisha kulipwa marupurupu ya shilingi milioni moja nukta tano na pesa zao za uzeeni shilingi elfu 30 kila mwezi kwa madiwani hao wa zamani lakini hadi kufikia sasa hawapokea haki yao.

Wakiongozwa na mwakilishi wao Peter Oduor katika ukumbi wa Tononoka mapema leo, wametoa wito kwa serikali kuharakisha na kuhakikisha wanalipwa marupurupu yao wanayodai baada ya kuhudumia serikali.

Kwa upande wake mwenyekiti wa muungano huo Mwalimu Mohammed ameiomba serikali kuu kuingilia kati suala hilo kuhakikisha madiwani wao wanalipwa pesa zao na kujiendeleza kimaisha.

Ameongeza kuwa pesa hizo zimechukua muda mrefu hata baadhi yao wamefariki.