Mgombea wa kiti cha ugavana kwa chama cha UDA kaunti ya Kilifi Esha jumwa amewaahidi wananchi kuwa ataimarisha maendeleo ili kukabiliana na umaskini.

Akiwahutubia wanawake wa kiislamu katika  eneo la mtaani mjini Kilifi Esha ameahidi kuanzisha hazina maalumu ya kifedha kwa wanawake ambayo watatumia kuimarisha biashara na miradi yao.

Mgombea huyo amebaini kuwa fedha hizo zitakuwa zikipewa wanawake bila riba yoyote ili waweze kujiimarisha kimaisha.

Naye mgombea wa kiti cha  wadi ya sokoni mjini humo Athman Matano amesema kuwa atashirikiana na Esha jumwa pindi tu atakapochaguliwa kuwa mwakilishi wa wadi hiyo.

Kulingana na Matano mji wa Kilifi unapaswa kupata kiongozi ambaye ataleta maendeleo katika sekta mbalimbali hasa sekta ya uvuvi,ardhi miongoni mwa sekta zengine.