Gavana wa kaunti ya Kwale Salimu Mvurya amepeana hotuba yake ya mwisho katika bunge la kaunti akisema kuwa imekua heshima kubwa kupewa nafasi kutumikia wakaazi wa Kwale kwa mihula miwili mfululuzo.

Katika hotuba yake zaidi amezungumzia mafanikio aliyoweza kutekeleza kwa hatamu mbili alizoongoza kutoka mwaka 2013 akipigia mfano kuboresha sekta ya elimu kwa mradi wa elimu ni sasa ambapo wanafunzi wamefadhiliwa 7,885 kutoka shule za kitaifa, elfu sabini na tano katika shule za kaunti na walio vyuo vikuu wakiwa 4,035.

Vilevile ameangazia ujenzi wa chuo cha walimu na shule za chekechea 929 kutoka chekechea 23 na uajiri wa walimu akitaja kuwa elimu ndio nguzo kuu ya maendeleo.

Vilevile ameweka wazi kuwa katika uongozi wake amejizatiti kuboresha sekta ya afya, na kuboresha miundo mbinu mbalimbali.

Kwa upande wake spika wa bunge hilo Sammy Ruwa amepongeza uongozi wa Mvurya akiutaja wenye manufaa kwa wakwale.