Wito umetolewa kwa viongozi katika Jamii na jamii kwa ujumla kushirikiana ili kuona kuwa suala la wanafunzi kujihusisha na visa vya uhalifu hapa Mombasa linakomeshwa.

Akitoa wito huo mgombea wa ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amesema ukosefu wa ajira hauwezi kuwa kisingizio cha visa vya uhalifu kwa wanafunzi shuleni bali ni tatizo la kijamii.

Aidha kutatua tatizo hilo Nassir amesema lazima kuwepo na ushirikiano mzuri baina ya viongozi wa kisiasi,viongozi wa kijamii na hata jamii kwa ujmla.

Vilevile Nassir ameeleza haja ya serikali ya kaunti ijayo kukodisha watoaji nasaha watakaoweza kuwapa nasaha na mwelekeo mzuri vijana ili kuunda vizazi bora siku za usoni.

Haya yanajiri huku Nassir akiwasihi vijana kutokubali kushawishiwa kuingia katika tabia potofu.