Viongozi katika kaunti ya Kilifi wameahidi kuimarisha raslimali za pwani ili kukabiliana na umaskini na kuenua uchumi.

Mgombea wa ugavana katika kaunti hiyo kwa chama cha PAA wakili George Kithi amesema  miongoni mwa raslimali ambazo zinapaswa kuboreshwa ni kurudisha shuhuli za bandari ya Mombasa na pia kufufua viwanda vilivyosambaratika miaka mingi iliyopita.

Akiwahutubia wananchi katika maeneo ya Matsangoni,Ganda na Kakuyuni Kithi amesema kuwa muda umefika wa wapwani kujikomboa.

Amebaini kuwa viwanda ambavyo atavifufua pindi tu atakapopata uongozi wa kaunti ya Kilifi ni kiwanda cha korosho ambacho amesema kuwa kitabuni nafasi zaidi za ajira.

Agenda za mgombea huyo zinaendelea kuungwa mkono na wanananchi wengi wa Kilifi huku wakiahidi kumpigia kura kwenye uchaguzi mkuu ujao.