Wananchi katika eneo la Gede eneo bunge la Kilifi kazkazini  wamenufaika na matibabu ya bure kutoka kwa wakfu wa George Kithi Foundation.

Wakfu huo  umechukua hatua hiyo ili kuwapa matibabu wananchi ambao hawawezi kumudu matibabu hasa katika magonjwa ambayo yanahitaji fedha nyingi ya kutibiwa.

Mwenyekiti wa wakfu huo wakili George Kithi amesema kuwa lengo la matibabu hayo ya bure ni kuimarisha afya na pia kurudisha shukrani kwa jamii.

Miongoni mwa magonjwa ambayo yamechungungwa kwa wananchi waliohudhuria matibabu hayo ni magonjwa ya msukumo wa damu,Kisukari,miongoni mwa magonjwa mengine.

Mama Sidi Kitsao ambaye amehudhuria matibabu hayo amepongeza hatua ya wakfu huo na kueleza kuwa umekuwa wa manufaa kwa afya yake.

Kulingana na Sidi hospitali zote za umma zinapaswa kuimarisha huduma za matibabu ili wananchi wasiojiweza waweze kupata matibabu bora.

Wakili Kithi ambaye anagombea kiti cha ugavana katika kaunti hiyo ameahidi kuboresha sekta ya afya pindi tu atakapochaguliwa kuwa gavana wa kaunti hiyo ya Kilifi.