Wananchi katika kaunti ya Kilifi watapata afueni ya kuwafundisha watoto wao baada ya mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti hiyo  wakili George Kithi kuahidi kuimarisha elimu.

Akiwahutubia wananchi katika eneo la Watamu,Kithi amesema kuwa lengo kuu ni kuhakikisha kuwa mgao wa fedha za masomo katika kaunti hiyo umeongezwa maradufu.

Kulingana na Kithi mgao huo utaongezwa kutoka milioni mia tatu hamsini mpaka milioni mia saba.

Kahindi kazungu mkazi wa eneo hilo amesema kuwa watoto wengi wamekosa kuendeleza masomo yao kwa ukosefu wa karo na hatua ya kiongozi huyo inapaswa kuungwa mkono na wananchi wote.

Kazungu pia amemtaka Kithi kuhakikisha kuwa fedha hizo za kimasomo zimegawanywa vyema bila upendeleo ili kuwafaidi wanafunzi wote.

Wakili Kithi pia amewataka wananchi kuhakikisha  kuwa wameimarisha miradi yao pindi tu atakapoanza kuwapa fedha za kimasomo watoto wao.