Wazee wa kaya katika kaunti ya Kilifi wameapa kuwaunga mkono viongozi wanaojali maslahi ya wapwani.

 Wazee hao wakiongozwa na kiongozi wa kayafungo thayari Mwaringa wamesema kuwa wanamuunga mkono wakilifi George Kithi katika azma yake ya ugavana katika kaunti hiyo.

 Kwenye hafla ya kumtawaza rasmi wakili Kithi katika azma hiyo,Mzee thayari amemtaka Kithi kutoogopa na kupigania swala la ardhi bila woga wowote.

 Naye wakili Kithi amewaahidi wazee hao kuwa atahakikisha kuwa swala la ardhi atalitatua vyema pindi tu atakapopata uongozi.

 Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa makaya katika kaunti hiyo.