Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama wa barabarani NTSA, imesitisha shughuli zote za kampuni ya mabasi ya Modern Coast, siku moja baada ya ajali iliyohusisha moja ya mabasi yake kuua abiria 33, na wengine 11 kuachwa na majeraha katika daraja la Nithi.

Katika taarifa siku yake, NTSA imesema kampuni hio yenye mabasi 31 imezuiwa kufanya uchukuzi baada ya ajali hiyo mbaya.
Kusitishwa kwa shughuli kutaathiri angalau njia saba ambazo kampuni inasafirisha aabiria.

Kulingana na ripoti, basi hilo lilikuwa likisafirisha abiria kutoka Maua kuelekea Mombasa kabla ya ajali hiyo ya saa kumi na mbili unusu jioni katika daraja la Nithi.