Usafiri umekwama baada ya wadau wa sekta ya usafiri na wakaazi wa Miritini eneo bunge la Jomvu kufunga bara bara ya Miritini wakilalamikia ubovu wa bara bara hiyo.

Wamelalamikia utepetevu wa Kenha kwamba wamekuwa wakifanya kazi kwa mwendo wa kombe huku wananchi na magari yakiharibika mara kwa mara.

Aidha wametoa makataa ya siku mbili Kenha kutatua tatizo hilo vinginevyo wamedai kufunga tena bara bara hiyo.

Mhandisi Peter Maruti amewahakikishia wakaazi hao wa Miritini kwamba mkandarasi atafanya kazi hiyo haraka iwezekanavyo huku akimtaka mbunge wa jomvu kuingilia kati na kusukuma hoja hiyo bungeni.

Kwa upande wake mbunge wa Jomvu Badi Twalib amehoji kwamba atakuwa akifuatilia kazi inavyo tekelezwa ili kuona kuwa watu wa miritini hawatatizwi tena na bara bara hiyo.