Wanahabari wa kike wa kiisalmu jijini Mombasa wamemshtumu waziri wa elimu proffesa George Magoha baada ya kumhusisha mwanahabari wa runinga ya NTV na kundi la Alshabab.

Wanahabari hao wakiongozwa na Mariam Kamau kutoka Radio Rahma, wamemtaka waziri Magoha kuomba msamaha mwanahanari huyo na wanawake wa kiislam kwa ujumla.

Mariam amemtaka Magoha kutomuhukumu mwanamke wa kiislamu kutokana na mavazi yake.

Kauli ya Maraim imetiliwa mkazo na mkurugenzi wa shirika la kuteta haki za wanawake la Sisters for Justice, Naila Abdallah.

Naye afisa wa kutoka shirika la Haki Afrika Mesaidi Omar amewataka viongozi kutokejeli jamii kwa misingi ya dini na ukabila wakati huu taifa linapokaribia uchaguzi.