Muungano wa Kenya Kwanza umepinga madai kuwa naibu wa raisi Dkt.William Ruto alilipwa ili kumuunga mkono Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa mwaka 2017.

Hapo jana Mkurugenzi mtendaji wa Azimio la Umoja Raphael Tuju alidai kuwa Naibu Rais William Ruto alilipwa kuunga mkono azma ya Uhuru Kenyatta ya urais.

Mbunge wa Nyali Mohamed Ali ameitaja kauli hiyo kuwa propaganda za kumuharibia Ruto sifa.Amewataka Tuju na wenzake wa mrengo wa Azimio kuuza Sera badala ya kukashifu viongozi wengine.

Kuhusu swala bandari ya Mombasa na reli ya kisasa mfuasi wa muungano wa Kenya Kwanza Njeri Kamau ametaja kuwa alipoteza ajira baada ya utendakazi wa bandari ya Mombasa kuhamishwa hadi Naivasha.

Njeri ambaye alikuwa akifanya kazi ya kusafirisha makasha,ametaja kuwa anapitia changamoto ya maisha baada ya kupoteza ajira.

Kufuatia kilio hicho,Mrengo wa Kenya Kwanza umeshikilia kuwa utarudisha huduma za bandari pindi tu Ruto akichaguliwa raisi.