Mgombea wa ugavana kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amemtaka waziri wa elimu profesa George Magoha kuomba msamaha au kujiuzulu kufuatia matamshi yake ya hivi majuzi yaliyoonekana kumbagua mwanahabari wa kislam na kumfananisha na kundi la kigaidi la Al-shabaab.

Akizungumza hapa Mombasa Nassir amekariri kuwa bunge la kumi na mbili limekuwa mstari wa mbele kubuni sheria za kuwaunganisha wananchi na kusema kuwa matamshi aliyoyatoa Magoha hayafai.

Nassir anamtaka Magoha kujiuzulu au kuomba msamaha huku akiwarai viongozi kuepuka kutumia kauli za ovyo za kuwagawanya wakenya.