Rais Uhuru Kenyatta amemkashifu naibu wake William Ruto na washirika wake kwa kueneza madai kuwa amewatishia maisha.

Uhuru akizindua barabara kuu ya Nairobi alimwambia Ruto kuzingatia kuuza ajenda zake, badala ya kueneza kile alichokiita "uongo".

Kauli ya Uhuru inajiri baada ya Ruto kumshutumu siku ya Ijumaa kwa kutoa vitisho dhidi yake.Ruto alisema rais alikuwa na mkutano wa faragha ambapo alimtishia yeye na washirika wake.