Serikali imeamrisha shule zote kufungwa kuanzia hapo kesho Agosti 2 mwaka huu.

Katika taarifa yake, Waziri wa elimu profesa George Magoha amesema shule zitabaki kufungwa hadi Agosti 11 mwaka huu.

Hii ni ili kupisha maadalizi ya zoezi la uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 9 mwaka huu.

Ikiwa kutakuwa na kuruduliwa kwa uchaguzi mkuu basi tarehe hizo huenda zikabadilishwa hatua itakayoathiri mitihani ya kitaifa inayotarajiwa kufanywa mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa kawaida shule na taasisi za elimu hutumiwa kama vituo vya kupigia kura kila msimu wa uchaguzi.Takriban shule 250 zitatumiwa kama vituo vya upigaji kura.