Vijana wameshauriwa kutotumiwa na wanasiasa kuzua vurugu wakati huu uchaguzi mkuu unakaribia.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kutetea haki za walemavu la Tunaweza Women With Disability,Charity Chahasi,amewataka vijana kujitenga na viongozi wanaopanga kuzua vurugu.

Wakati huo huo amekemea vikali vurugu zilizoshuhudiwa katika eneo la Nyali baina ya wafuasi wa Mbunge wa Nyali Mohammed Ali na Said Abdalla maarufu Saido

Amewataka viongozi hao kufanya kampeni za amani na kukoma kuchechea vurugu.