Wizara ya afya imesema Kenya bado haijaripoti kisa chochote cha Ebola.

Wizara, hata hivyo, imeorodhesha kaunti 20 kati ya 47 kuwa kaunti zilizo hatarini zaidi.

Ni pamoja na Busia, Nakuru, Kiambu, Nairobi, Kajiado, Machakos, Makueni, Taita Taveta, Mombasa, Kwale, Kericho, Bungoma, Siaya, Migori, Homa Bay, Kisumu, Trans Nzoia, West Pokot, Turkana na Uasin Gishu.

Mkurugenzi mkuu katika wizara ya afya daktari Patrick Amoth,hata hivyo, amesema hakuna mpango wa kusimamisha safari za ndege kutoka Uganda lakini wizara badala yake imeongeza ufuatiliaji na uchunguzi katika maeneo ya mipakani na sehemu zote za kuingia.

Takwimu kutoka kwa wizara hiyo zinaonyesha watu 18, 726 walichujwa katika vituo mbalimbali vya kuingia kati ya Septemba 20 na 25.