Washikadau wanaohusika na maswala ya watoto kaunti ya Taita Taveta wametakiwa kutoa hamasa kwa walimu,wazazi na jamii kwa jumla kuhusu haki za watoto.

Akizungumza mjini Voi mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za kibinadamu la sauti ya wanawake Makrina Mwamburi amesema kuwa idadi kubwa ya jamii haina ufahamu wa haki za watoto jambo linalochangia haki nyingi za watoto kukiukwa.

Makrina ameongeza kuwa kupitia hili visa vingi vya dhulma kwa watoto huenda vikapungua.

Mwamburi amesema kuwa kwa sasa jamii imejitokeza kuripoti visa vya dhulma tofauti hasa zile za kijinsia na hii ni kutokana na hamasa zinazofanywa na mashirika tofauti ya kijamii eneo hilo.