Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ametoa Wito kwa viongozi wa utumishi nyanjani kushirikiana na serikali ya kaunti ili kukabiliana na visa vya utumizi wa mihadharati.

Akizungumza mapema Leo afisini mwake na viongozi hao Gavana Nassir amesema ni sharti kuwepo na mipangilio mwafaka ya kuwahamisisha vijana dhidi ya athari ya dawa za kulenya.
 
Kulingana na Nassir vijana wengi hapa Mombasa wameingilia uraibu hali ambayo mara nyingi inapelekea utovu wa Usalama.
 
Aidha Nassir ameeleza haja ya kuwepo kwa ushirikiano baina viongozi wa utumishi nyanjani na serikali ya kaunti kutoa hamasa kwa jamii dhidi ya athari za utumizi wa mihadharati.