Biashara haramu ya wanyama pori, uharibifu wa maeneo ya wanyamapori wanamoishi na kupotea kwa maeneo ya vyanzo vya maji ni miongoni mwa tabia zinazoharibu mazingira ya viumbe hai nchini.

Haya yalisemwa na Daktari Judith Nyunja, mwanasanyasi mkuu wa utafiti kutoka taasisi ya utafiti wa maeneo ya maji na mafunzo ya wanyamapori nchini.

Akizungumza na wanahabari wanaoangazia habari za Sayansi kutoka kwa kikundi cha wanahabari Mesha kwa njia ya mtandao, Daktari Judith aliongeza kusema kuwa ukulima mbaya pia unasababisha maeneo mengi ya vyanzo vya maji kukauka ama kupungua.

Zaidi alisema kuingiliwa kwa maeneo ya wanyamapori kutokana na shughuli za kibinadamu hasa kwa kuzungushwa singenge mashamba hayo akitolea mfano eneo la Masai Imara ambalo limeathiri vibaya.

Alisema kwa kufanya hivyo,njia za wanyama pori zinafungwa na kuharibu mazingira yao hivyo basi kuwasababishia msongo wa mawazo.

Kutokana na hayo, Daktari Judith alisema kiwango cha wanyamapori kimepungua katika ikolojia ya Savanna kwa kipindi cha mwaka 1977-2016 kwa asilimia 68.

Daktari Judith alitoa wito kwa jamii kuhakikisha kuwa wanalinda mazingira ili kuunda mfumo wa ikolojia unaostahimili.